Swali: Katika miji ya magharibi baadhi ya misikiti iko kwenye nyumba za kupanga. Ndani ya misikiti hii kunaswaliwa swalah tano na Ijumaa. Pamoja na hivyo kuna baadhi ya waislamu ambao wanaishi jirani ya msikiti huu na wanaona kuwa ni jambo halikuwekwa kwenye Shari´ah kuswali kwenye msikiti huu kwa kuwa ni nyumba za kupanga na sio milki ya wenye kuswali. Je, maneno haya ni sahihi?

Jibu: Huyu hataki kuswali pamoja na mkusanyiko. Anatafuta udhuru. Ni nani kakwambia kuwa haijuzu kuswali mahala ambapo ni pa kupanga? Ni nani kakwambia hivi? Inajuzu kuswali mahala popote ambapo kumeandaliwa kwa ajili ya swalah, sawa ikiwa ni pa kupanga au si pa kupanga. Kupanga huku ni kwa ajili ya haja na dharurah katika miji ya makafiri na miji ya magharibi. Hichi ni kitendo kizuri.

Lakini mtu huyu hataki kuswali pamoja na mkusanyiko sasa ndio maana anatafuta udhuru huu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (42) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-3-22.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020