“Allaah” na “Muhammad” kwenye kuta za misikiti

Swali: Baadhi ya Misikiti wanaweka “Allaah” upande wa kulia wa Mihrab na “Muhammad” upande wake wa kushoto. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Hili halijuzu. Hili ni jina la Mtume likiwa pamoja na Allaah (Jalla wa ´Alaa). Baadhi yao huweka “Ee Allaah!” na “Ee Muhammd!”. Wengine huweka “Allaah”, “Muhammad”. Yote haya hayajuzu.

Asli ya kuandika kwenye misikiti haijuzu, sawa ikiwa ni Aayah za Qur-aan au mambo mengine. Misikiti isiwashughulishe wenye kuswali na wala isiwe na mapambo. Misikiti haikujengwa kwa ajili ya haya. Msikiti ni nyumba ya kufanyia ´ibaadah. Haikujengwa kwa ajili ya mapambo.

Kuandika “Allaah” upande wa Mihrab na”Muhammad” upande mwingine, hili halijuzu.

Baraza za kufutu limetoa fatwa kuhusu kuondosha mambo haya. Haijuzu kufanya hivi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (42) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-3-22.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020