Swali: Je, inafaa kwa mtu kuswali kichwa wazi?

Jibu: Inajuzu kwa mtu kuswali pasi na kuwa na kitu kichwani mwake. Sio faradhi kufunika kichwa wakati wa kuswali. Kwa hiyo mtu akiswali kichwa wazi swalah yake ni sahihi. Hata hivyo bora ni kukifunika akiwa baina ya watu wenye mazowea ya kufunika vichwa vyao, kwa saabu Allaah amesema:

يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ

“Enyi wana wa Aadam! Chukueni mapambo yenu wakati wa kila swalah.”[1]

Akiwa baina ya watu wanaofunika vichwa vyao, basi bora ni yeye pia kufunika kwa sababu ni miongoni mwa mapambo yaliyoamrishwa na Allaah.

[1] 7:31

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/294-295)
  • Imechapishwa: 03/05/2026