Kuswali katika safu kati ya watoto wawili

Swali: Swalah ya mtu ambaye kishabaleghe kati ya vijana wawili wadogo inazingatiwa ni kama aliyeswali peke yake kwenye safu?

JIbu: Ikiwa wamefikia upeo wa kuweza kupambanua ni sawa. Inajuzu kufanya safu na vijana wenye upeo wa kupambanua. Ama ikiwa hawajafikia upeo wa kuweza kupambanua, asiunge nao safu kwani anazingatiwa kuwa peke yake kwenye safu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (78) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/taf_3_1_1433.mp3
  • Imechapishwa: 22/08/2020