Kuswali kamili au kwa kupunguza katika siku ya Tarwiyah?

Swali: Je, Sunnah kuswali swalah kamili au kufupisha siku ya Tarwiyah?

Jibu: Ni kufupisha swalah kuwa Rak´ah mbili, kama alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) siku ya Tarwiyah.

Swali: Ikiwa wako katika kundi na hawawezi kusikia Khutbah ya imamu. Je, mmoja wao anaweza kuwahutubia?

Jibu: Hakuna tatizo. Ikiwa wanaswali pamoja, mmoja wao anaweza kuwakhutubia khaswa ikiwa miongoni mwao kuna mwanafunzi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24999/هل-المشروع-يوم-التروية-الاتمام-ام-القصر
  • Imechapishwa: 24/01/2025