Kusoma Qur-aan ijumaa kabla ya imamu kuingia ni Bid´ah

Swali: Je, ni halali msomaji akasimama siku ya ijumaa kabla ya imamu kuja na akija msomaji anakaa na baada ya hapo Khatwiyb anatoa Khutbah? Je, ni miongoni mwa adabu za ijumaa na Sunnah zake au ni katika Bid´ah munkari?

Jibu: Hatujui dalili yenye kufahamisha msomaji akasimama na kusoma Qur-aan siku ya ijumaa kabla ya imamu kuingia na watu wakamsikiliza na imamu akiingia msomaji anaacha kusoma. Asli katika ´ibaadah ni kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kufanya kitendo kisichokuwa ndani yake dini yetu, basi atarudishiwa mwenyewe.”

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/357-358)
  • Imechapishwa: 23/08/2020