Kusoma kwa sauti katika Rak´ah ya mwisho ya Maghrib

Swali: Kuna mtu aliingia msikitini ili aswali Maghrib na akawahi Rak´ah mbili pamoja na imamu na akaswali Rak´ah ya mwisho peke yake. Je, asome kwa sauti ya juu katika Rak´ah hii na asome Suurah “al-Faatihah” kwa kuzingatia kwamba aliswali Rak´ah ya mwisho pamoja na imamu au hiyo Rak´ah aliyoiwahi pamoja na imamu inazingatiwa ni ya pili?

Jibu: Hiyo Rak´ah ambayo alikidhi baada ya imamu kutoa Tasliym inazingatiwa ni Rak´ah ya mwisho. Kwa hiyo haikusuniwa kusoma kwa sauti ya juu. Kwa sababu maoni sahihi ya wanazuoni ni kwamba ile sehemu ya swalah aliyowahi yule ambaye amekuja amechelewa inazingatiwa ndio sehemu yake ya mwanzo ya swalah na ile anayolipa ndio sehemu yake ya mwisho. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kunapokimiwa swalah basi msiiendee hali ya kukimbia bali iendeeni kwa kutembea. Lazimianeni na utulivu. Kile mtakachowahi, kiswalini, na kile mtachokosa basi kikamilisheni.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/240)
  • Imechapishwa: 29/10/2021