Swali: Kusema “Subhaan Allaah”, “Alhamdulillaah” na “Allaahu Akbar” baada ya kila faradhi inakuwa bora kwa vidole vya mkono wa kulia au kwa vidole vya mikono yote miwili pamoja?

Jibu: Bora ni hayo yafanyike kwa mkono wake wa kuume. Kwa sababu imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alikuwa akihesabu kwa mkono wake wa kuume. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anapenda kuanza kwa upande wa kulia wakati wa kuvaa kwake viatu, kuchana nywele zake, kujitwahirisha kwake na katika mambo yake yote.”

Lakini inafaa kuhesabu kwa vidole vyote. Kwa sababu imepokelewa katika baadhi ya Hadiyth yanayofahamisha juu ya hayo kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Vitaulizwa na kutamkishwa.”

Kwa hayo inapata kufahamika kwamba jambo hili ni lenye wasaa na kwamba haitakikani kufanya ugumu na kugombana juu ya jambo hili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/187)
  • Imechapishwa: 29/10/2021