Kusimama kabla ya kumaliza Adhkaar za baada ya swalah

Swali: Je, kumepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Hadiyth yoyote inayosema kuwa mja akimaliza kuswali asisimame kutoka mahali pake mpaka amalize kufanya Dhikr?

Jibu: Sijafikiwa na kitu. Hata hivyo kufanya hivo ndio bora akamilishe kwanza zile Dhikr zilizowekwa katika Shari´ah.

Swali: Lakini sio kwa njia ya ulazima?

Jibu: Hapana, sio kwa njia ya ulazima. Akitoa salamu amemaliza kuswali.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23367/ما-حكم-القيام-بعد-الصلاة-قبل-اكمال-اذكارها
  • Imechapishwa: 04/01/2024