Kushuka kwa Allaah usiku wa nusu ya Sha´baan kupitia upokezi wa ´Aaishah


89 – Muhammad bin Yahyaa bin Haaruun al-Askaafiy ametuhadithia: ´Abdah bin ´Abdillaah as-Swaffaar ametuhadithia …:

Pia al-Qaadhwiy al-Husayn bin Ismaa´iyl ametuhadithia: al-Fadhwl bin Abiy Twaalib ametuhadithia…:

Ibn ´Ubayd al-Qaasim bin Ismaa´iyl pia ametuhadithia: al-Hasan bin Muhammad as-Swabbaah na al-Hasan bin Yahyaa al-Jurjaaniy ametuhadithia…:

Pia Abu Bakr an-Naysaabuuriy ametuhadithia: Muhammad bin ´Abdil-Malik ametuhadithia: Yaziyd bin Haaruun ametuhadithia: al-Hajjaaj ametuhadithia, kutoka kwa Yahyaa bin Abiy Kathiyr, kutoka kwa ´Urwah, kutoka kwa ´Aaishah ambaye amesema:

“Usiku mmoja nilimkosa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Nikatoka na tahamaki nikamuona yuko al-Baqiy´ hali ya kuwa amekinyanyua kichwa chake kukielekeza mbinguni. Akanambia: “Je, ulikuwa unaogopa kwamba Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) watakudhulumu?” Nikasema: “Nini, ee Mtume wa Allaah?” Nilidhani kuwa umewaendea baadhi ya wake zako.” Akasema: “Hakika Allaah (´Azza wa Jall) hushuka katika mbingu ya chini ya dunia usiku wa nusu Sha´baan na akasamehe zaidi ya wingi wa nywele za Kalb cha kondoo.”[1]

Matamshi yao ni yenye kukaribiana.

[1] al-Hajjaaj bin Artwa´ah alikuwa anafanya Tadliys. Hapa amesimulia pasi na kubainisha namna gani.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 169-170
  • Imechapishwa: 12/01/2021
  • mkusanyaji: ´Allaaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy