Kushuka kwa Allaah usiku wa nusu ya Sha´baan kupitia upokezi wa ´Aaishah 02


90 – Ismaa´iyl bin ´Abbaas al-Warraaq ametuhadithia: al-´Abbaas bin Muhammad ametuhadithia: ´Umar bin Hafsw bin Ghiyaath ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia: kutoka kwa Hajjaaj, kutoka kwa Yahyaa bin Abiy Kathiyr, kutoka kwa ´Urwah, kutoka kwa ´Aaishah aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Usiku wa nusu Sha´baan Allaah (´Azza wa Jall) hushuka katika mbingu ya chini ya dunia na akasamehe madhambi mengi zaidi ya nywele za Kalb cha kondoo.”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 170
  • Imechapishwa: 12/01/2021