Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa Abu Sa´iyd na Abu Hurayrah 10

61 – ´Abdus-Swamad bin ´Aliy ametuhadithia: Ja´far bin Ahmad bin al-Khaliyl ametuhadithia: ´Abdus-Salaam bin ´Aaswim ametuhadithia: Abu Zuhayr ametuhadithia: Jaabir bin Yahyaa al-Hadhwramiy ametuhadithia, kutoka kwa Abu Ishaaq, kutoka kwa al-Agharr, kutoka kwa Abu Hurayrah na Abu Sa´iyd al-Khudriy:

“Nawashuhudilia kuwa wamesema na wao wanashuhudia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Allaah anatoa muhula mpaka kunapopita theluthi ya usiku ya kwanza ndipo hushuka katika mbingu ya chini kisha ananadi: “Je, kuna mtenda dhambi? Je, kuna mwenye kuomba msamaha? Je, kuna mwenye kuuliza? Je, kuna mwenye kuomba?”

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hawakusanyiki watu wakimdhukuru Allaah (´Azza wa Jall) isipokuwa wanazungukwa na Malaika, huteremkiwa na utulivu, hufunikwa na rehema na Allaah anawataja kwa wale walioko Kwake.”

al-A´mash ameipokea pia kutoka kwa Abu Ishaaq na Habiyb bin Abiy Thaabit kutoka kwa al-Agharr, kutoka kwa Abu Hurayrah.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 135-136
  • Imechapishwa: 26/04/2020