Kushirikiana na kusameheana – ishara ya al-Ikhwaan al-Muslimuun


Swali: Baadhi ya waalimu wanaotufunza katika vyuo vikuu vyetu wanasema kuwa kila kundi la waislamu lina mambo yake mazuri na kuwahimiza wanafunzi wayachukue mambo hayo. Wamepigia mfano wa Jamaa´at-ut-Tabliygh na Suufiyyah katika njia zao za kulingania. Je, ni kweli?

Jibu: Kama mnavojua wako na kanuni wanayoiita “Kanuni ya kidhahabu” na inasema ifuatavyo:

“Tushirikiane katika yale tunayoafikiana na tupeane udhuru katika yale tunayotofautiana.”

Maoni haya yametokana na kanuni hii. Hapana, haijuzu. Haitakiwi kupeana udhuru katika yale mambo tunayotofautiana, isipokuwa tunatakiwa kurudi katika dalili. Yule ambaye anayo dalili basi yeye ndiye mwenye haki na mwenye kupatia. Yule ambaye anakwenda kinyume na dalili basi ni mwenye kukosea. Haturidhii makosa. Hatupakani mafuta katika dini ya Allaah (´Azza wa Jall). Yale yanayokwenda kinyume na dalili ni yenye kurudishwa nyuma. Hatufuati isipokuwa yale yanayoafikiana na dalili, pasi na kuja yametoka kwa nini. Haki ni kitu kilichompotea muumini; pale anapokipata basi anakichukua. Ama kusema kwamba tuwe marafiki na kusameheana na kushirikiana katika yale mambo tunayoafikiana na kupeana udhuru katika mambo mengine – tupeane udhuru pindi tunapomwomba mwingine asiyekuwa Allaah? tupeane udhuru pindi tunayaabudu makaburi na makuba? Ni yepi ambayo tunaafikiana? Tunaafikiana juu ya jina ´Uislamu´ peke yake. Haitoshi. Uislamu ni lazima uhakikishwe. Kanuni hii ni batili. Wanaiita kuwa ni “Kanuni ya kidhahabu”. Kwa masikitiko makubwa wanaikumbatia baadhi ya vijana na Hizbiyyuun. Ni kanuni ya batili inayokwenda kinyume na Qur-aan  na Sunnah. Allaah hakutwambia tupeane udhuru; bali amesema:

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا

“Mkizozana juu ya jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa mnamuamini Allaah na siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri kabisa.”[1]

Hakusema kwamba tupeane udhuru na kwamba kila mmoja abaki katika ´Aqiydah yake.

[1] 04:59

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Fatwaa al-Hamawiyyah (35)
  • Imechapishwa: 11/09/2020