Amesimama kukamilisha swalah yake kabla ya Tasliym ya pili ya imamu


Swali: Ni zipi nasaha zako kwa ambaye amepitwa na Rak´ah moja au zaidi kisha akasimama kukamilisha swalah yake kabla ya imamu kutoa salamu ya pili?

Jibu: Hili ni kosa. Lakini baadhi ya wanachuoni wanaona kuwa swalah yake inasihi. Jopo la wanachuoni wengi wanaona ulazima wa salamu ya kwanza. Makusudio ni kwamba anapaswa kusubiri mpaka pale ambapo imamu atatoa salamu ya pili kwa ajili ya kujiondoa nje ya tofauti za wanachuoni. Kwa sababu wako wanachuoni wenye kuona kuwa swalah yake haisihi na kwamba  salamu ya pili ni lazima.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (15)
  • Imechapishwa: 11/09/2020