Kusafiri kwa ajili ya kwenda kutoa pole

Swali: Ni jambo limewekwa katika Shari´ah kusafiri kwa lengo la kwenda kutoa pole kwa ajili ya maiti?

Jibu: Hapana. Halikuwekwa katika Shari´ah. Hakuna haja ya kusafiri. Wape pole kwa simu na wewe uko mahala pako na wala hakuna haja ya kusafiri.

Swali: Ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwa wale wafiliwa kuwatengenezea chakula wale waliokuja kutoa pole?

Jibu: Hapana. Wafiliwa wapike chakula cha kwao wao wenyewe na si kuwapikia wageni. Mambo yanatakiwa kuwa kinyume. Lililo la wajibu ni wao ndio wanaotakiwa kutengenezewa na kuletewa chakula.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (86) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/NEW.lite_.mp3
  • Imechapishwa: 14/07/2018