Kiwango cha chini cha Qur-aan kwa siku

Swalii: Ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwa kila muislamu kusoma juzu kutoka katika Qur-aan ili aweze kuikhitimisha kwa mwezi?

Jibu: Ndio, kwa uchache. Angalau kwa uchache kila mwezi akhitimishe mara moja. Lau atakhitimisha kila baada ya siku kumi au kila baada ya siku tatu, kama walivokuwa wakifanya Salaf, ndio bora na vyema zaidi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (86) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/NEW.lite_.mp3
  • Imechapishwa: 14/07/2018