Kupokea malipo au zawadi wakati wa kupeana damu

Swali: Ni ipi hukumu ya kupokea malipo wakati wa kujitolea damu?

Jibu: Damu haiuzikani. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza mtu kuuza damu yake na thamani yake hiyo damu. Kwa hiyo utakapomzawadia mtu damu yako, basi usichukue chochote kutoka kwake kama malipo. Ni mamoja ulichochukua ni zawadi au chenginecho.

Tukikadiria kuwa umechukua chochote, basi kitoe swadakah kuwapa baadhi mafukara. Usikitumie wala usikile. Kwa sababu imethibiti kutoka Mtume wa Allaah (Swala Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amekataza thamani ya damu. Zawadi ni thamani pia. Hakukupa zawadi hiyo isipokuwa ni kwa ajili ya hiyo damu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4412/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D8%AE%D8%B0-%D8%A7%D9%84%D9%87%D8%AF%D8%A7%D9%8A%D8%A7-%D9%85%D9%82%D8%A7%D8%A8%D9%84-%D8%A7%D9%84%D8%AA%D8%A8%D8%B1%D8%B9-%D8%A8%D8%A7%D9%84%D8%AF%D9%85
  • Imechapishwa: 09/06/2020