Kupiga dufu masiku kadhaa kabla ya harusi

Swali: Mwanamke huyu anasema kuwa katika ada yao wakati wa ndoa kunakuwa na siku inayoitwa “siku ya hina” ambapo kunapakwa hina kabla ya siku ya ndoa kwa siku moja kabla. Je, ni jambo limewekwa katika Shari´ah kupiga dufu siku hii?

Jibu: Hapana, kupiga dufu inakuwa pale mume anapoingia kwa mke wake ile siku ya ndoa. Hii ndio sehemu ya kupiga dufu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (39) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-2-10.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020