Imependekezwa kula daku na kuichelewesha. Pia imependekezwa kukata swawm kwa tende pale tu jua linapozama.

Imependekezwa kuwa mkarimu zaidi katika Ramadhaan, kutenda mema mengi, wingi wa swadaqah, kwa sababu ya kumwigiliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Pia imependekezwa kuidurusu Qur-aan na kukaa I´tikaaf, na khaswa katika zile siku kumi za mwisho za Ramadhaan na kufanya bidii ya ziada. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Mtume  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ilikuwa zinapoingia zile siku kumi za mwisho basi hufunga vizuri kikoi chake, anahuisha usiku wake na anaiamsha familia yake.”[1]

Wanachuoni wamesema kwamba kufunga vizuri kunaweza kuwa na maana mbili:

1- Anawaepuka wanawake.

2- Ni kinaya cha kushamiri katika matendo. Wamesema kujipinda kwake katika matendo ilikuwa ni kwa sababu ya usiku wa Qadr.

[1] al-Bukhaariy (2024) na Muslim (1174).

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtaswar Minhaaj-il-Qaaswidiyn, uk. 44-45
  • Imechapishwa: 14/05/2020