Kupeana mkono na wanawake kwa ajili ya manufaa

Swali: Ni ipi hukumu ya kusalimiana kwa kupeana mkono na mwanamke wa kando kwa ajili ya manufaa?

Jibu: Hapana, haijuzu kusalimiana kwa kupeana mkono na wanawake. Lakini awazungumzishe bila kupeana nao mikono. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mimi sipeani mkono na wanawake.”

´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Naapa kwa Allaah Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakupatapo kamwe kugusa mkono wa mwanamke. Alikuwa akiwapa kiapo kwa maneno.”

Swali: Kuwatolea salamu?

Jibu: Kwa maneno:

السلام عليكم

“Amani iwe juu yenu.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwapitia wanawake ambapo akawatolea salamu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21928/حكم-مصافحة-المراة-الاجنبية-للمصلحة
  • Imechapishwa: 03/10/2022