Swali: Mwanamke kukata nywele zake kwa ajili ya kumpambia mume wake.

Jibu: Hapana vibaya akipunguza katika ncha. Lakini asinyoe. Akikata kidogo kwa sababu ni nyingi au ni ndefu sana zinamdhuru au mume akaona kuwa ukataji huo ndani yake unamsaidia au kunamfanya kuwa mzuri zaidi hapana vibaya.

Swali: Ni kipi kikomo cha ukataji wa mwanamke?

Jibu: Hakuna kikomo maalum. Sharti tu ni yeye asijifananishe na wanamme wala wanawake [wa kikafiri].

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21940/حكم-قص-شعر-المراة-للتجمل-لزوجها
  • Imechapishwa: 03/10/2022