Kupaka hina na kutengeneza nywele kwa anayetaka kuchinja siku ya ´Iyd-ul-Adhwhaa

Swali: Mwanamke anayetaka kuchinja Udhhiyah… kwa sababu kwetu huku baadhi ya mama na bibi zetu wa zamani wanatwambia kuwa tusipake hina isipokuwa baada ya kuchinja. Je, ni sahihi au ni ukhurafi tu?

Jibu: Hayo hayana msingi wowote. Hapana vibaya kupaka hina kwa anayetaka kuchinja. Hapana vibaya akajitia manukato. Hapana vibaya akapiga mswaki pale anapotaka. Sio haramu. Lakini asikate chochote katika nywele wala kucha zake unapoingia mwezi wa Dhul-Hijjah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Utapoingia mwezi wa Dhul-Hijjah na akataka mmoja wenu kuchinja, basi asikate kutoka katika nywele wala kucha zake chochote mpaka achinje kwanza.”[1]

Katika upokezi mwingine imekuja:

“… wala chochote katika ngozi yake.”

Kwa maana yule anayemchinjia, anamchinjia mtu katika familia yake au mzazi wake. Kama anamchinjia kwa kujitolea. Hapa ni pale ambapo unapoingia mwezi wa Dhul-Hijjah. Asikate wala asipunguze chochote katika nywele, kucha wala ngozi yake. Asikate chochote katika ngozi yake wala mwili wake mpaka achinje kwanza ima ile siku ya kwanza ya kuchinja au baada yake. Hayo ndio yamewekwa katika Shari´ah. Hata hivyo hapana neno akazifumua nywele zake, akazisafisha na akajipaka hina. Lakini asijichanue kwa kichanuo ili nywele zisikatike mpaka achinje. Licha ya hivo ni sawa akazisafisha na akazisugua. Yote haya hayana neno. Kilichokatazwa ni kuzikata kwa nguvu au kitu kingine.

[1] Muslim.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/6014/حكم-استعمال-الحناء-لمن-ارادت-الاضحية
  • Imechapishwa: 09/06/2024