Kuosha mikono wakati wa kuamka kutoka usingizini

Swali: Nikiamka usiku hali ya kuwa wudhuu´ wangu umechenguka na sikuosha mikono yangu mara tatu. Nikawa nimetawadha tu na kuswali. Kisha katikati ya swalah nikakumbuka hilo. Nifanye nini?

Jibu: Kuosha mikono wakati wa kumka ni jambo la wajibu kwa mujibu wa wanachuoni wengi. Ni jambo la wajibu. Lakini ukisahau na uliosha mikono yako yote vizuri wakati wa kutawadha, ulisahau kuanza kuiosha mwanzoni mara tatu kabla ya kuanza kutawadha – hili ni nje ya wudhuu´ – limepita pahala pake. Swalah yako na wudhuu´ wako ni sahihi – Allaah akitaka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (33) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-10-23.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020