Kumchinjia mtoto mchanga na kumpa jina ni haki ya nani?

Swali: Kutoa jina kumpa mtoto ni haki ya mume au mke au wote wawili?

Jibu: Kutoa jina kumpa mtoto ni haki ya baba yake. Yeye ndiye anatakiwa kumchagulia jina na kumfanyia ´Aqiyqah kwa kumchinjia. Hii ni haki ya mtoto juu ya baba yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (33) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-10-23.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020