Kuomba kwa kunyanyua mikono baada ya wudhuu´

Swali: Ni ipi hukumu ya kunyanyua mikono kwa ajili ya kuomba du´aa baada ya kutawadha?

Jibu: Hili halikuthibiti. Haikuthibiti kuwa mikono inanyanyuliwa baada ya kutawadha. Kilichothibiti ni yeye kuelekeza macho yake mbinguni na kusema:

أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّداً عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ

“Nashuhudia ya kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa pekee hana mshirika, na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na ni Mtume wake.”

اللَّهُمَّ اجْعَلْنِي مِنَ التَّوَّابِينَ وَاجْعَلْنِي مِنَ الْمُتَطَهِّرِينَ

“Ee Allaah! Nijaalie kuwa katika wenye kutubia na nijaalie kuwa katika wenye kujitwaharisha.”

Afanye hivo bila ya kunyanyua mikono.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (39) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-2-10.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020