Swali: Ni ipi hukumu ya kuogelea na kupiga mbizi?

Jibu: Kinachozingatiwa ni kusiwepo chochote kitachoshuka kwenye koo. Hata hivyo maji ya bahari yanatofautiana. Maji ya chumvi yanaweza kupenya kwa ndani. Niliogelea ndani yake. Yanapenya ndani ya koo pasi na mtu kujua hilo. Ninashauri kujiweka mbali na hilo. Maji matamu hayapenyi kwenye koo shingoni na kuna khatari nayo pia yakaweza kufanya hivo.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 80
  • Imechapishwa: 26/08/2020