Swali: Vipi kuoanisha kati ya maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth:

“… na tuzungumze haki popote tulipo pasi na kuchelea lawama za mwenye kulaumu.”

na kati ya kutanguliza manufaa katika suala la kuamrisha mema na kukataza maovu?

Jibu: Hii ni kazi ya mtawala. Mtawala ndiye anatakiwa kupanga mambo ili kusitokee vuguru na fitina.

Swali: Nakusudia mwamrishaji wa kawaida na mtu wa kawaida.

Jibu: Azungumze kutegemea na uwezo wake na kwa maneno mazuri:

ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ

“Lingania katika njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mazuri na jadiliana nao kwa ambayo ni mazuri zaidi.” (16:125)

Azungumze kwa maneno na vitendo vizuri. Huku ndio kukemea kwa mdomo. Akimuona anayeapa kwa asiyekuwa Allaah amwambie kumcha Allaah na kwamba haijuzu. Akimuona mwenye kutukana na kulaani amwambie kuwa haijuzu. Akimuona mwenye kuwatazama wanawake na anafanya matatizo ambayo kunakhofiwa juu yake amkemee. Akimuona anayekosa swalah ya mkusanyiko amnasihi na kadhalika.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21986/كيف-يجمع-بين-النصيحة-ومراعاة-المصلحة
  • Imechapishwa: 11/10/2022