Wakati ambapo mtu anakemewa hadharani kwa maovu yake

Swali: Kukataza maovu yanayofanywa hadharani kumeshurutishwa kufanya kwa siri kama ilivyoshurutishwa katika kutoa nasaha au maovu yanayofanywa hadharani yanakemewa hadharani bila kufanya kwa siri?

Jibu: Ikiwa amefanya kati ya watu anakemewa hadharani. Lakini kama amefanya kati yako wewe na huyo ambaye amefanya kitu hicho, basi utazungumza kati yako wewe na yeye na kumnasihi. Ama kama amefanya mbele ya watu atabainishiwa mbele ya watu ya kwamba kitendo hicho ni munkari na kwamba hakijuzu. Lengo ni ili asidanganyike mtu yeyote. Lakini ukimuona anafanya maovu basi unalazimika kumnasihi kati yako wewe na yeye. Ukimuona peke yake umkataze na kumwambia kuwa ni maovu na mfano wa maneno kama haya mazuri, njia nzuri na upole. Kama alivosema Mola wako:

ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ

“Lingania katika njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mazuri na jadiliana nao kwa ambayo ni mazuri zaidi.” (16:125)

Lakini kama anafanya hivo mbele ya watu mbainishie kuwa kitendo hicho ni maovu na kwamba hakijuzu. Kwa mfano anayevuta sigara mbele ya watu, anayekunywa pombe mbele ya watu, mtukanaji na mwenye kulaani. Watu sampuli hii wanakemewa hadharani.

Swali: Ninacholenga ni maovu ya kawaida yanayofanywa hadharani yanakemewa hadharani?

Jibu: Ndio, yakemee hadharani. Muda wa kuwa yamefanywa hadharani basi yanakemewa hadharani.

Swali: Hakukuwekwa sharti ya kufanya kwa siri?

Jibu: Watu wabainishiwe kuwa ni maovu. Ambaye anafanya maovu hadharani sokoni anakemewa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21989/ما-كيفية-انكار-المنكرات-العامة-المعلنة
  • Imechapishwa: 11/10/2022