Swali: Kunyoa ndevu ni katika madhambi makubwa?

Jibu: Ni maovu na maasi. Kusema kwamba ni dhambi kubwa, Allaah ndiye mjuzi zaidi.

Swali: Kuendelea kunyoa ndevu si kunaigeuza kutoka katika maasi kwenda katika dhambi kubwa?

Jibu: Ninachokusudia ni kwamba ni maasi. Kufuga ndevu ni lazima. Kuzipunguza au kuzinyoa ni katika maasi. Kusema kwamba ni dhambi kubwa ni jambo linahitaji utafiti mwingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23274/هل-حلق-اللحية-من-الكباىر
  • Imechapishwa: 16/12/2023