Swali: Kitendo chake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kinafuta maneno yake?

Jibu: Muda wa kuwa inawezekana kuoanisha haifuti isipokuwa kwa sharti mbili:

1 – Isiwezekane kuoanisha. Ni lazima ishindikane kukusanya.

2 – Historia iwe inatambulika.

Hizi ni miongoni mwa sababu za kukusanya. Ni sawa ikitambulika historia na isiwezekane kukusanya. Ni lazima kuoanisha ikiwezekana kukusanya au historia haitambuliki.

Swali: Wako wanaosema kuwa kitendo hakifuti maneno, kwa sababu kitendo…

Jibu: Kwa sababu kitendo kinafasiri na hakifuti. Kitendo kinafasiri.

Swali: Labda kitendo kinapelekea katika umaalum?

Jibu: Kitendo kinafasiri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23275/%D9%87%D9%84-%D9%81%D8%B9%D9%84-%D8%A7%D9%84%D9%86%D8%A8%D9%8A-%EF%B7%BA-%D9%8A%D9%86%D8%B3%D8%AE-%D9%82%D9%88%D9%84%D9%87
  • Imechapishwa: 16/12/2023