Kuacha kuhiji ilihali mtu ana uwezo

Swali: Je, ni dhambi kubwa kuacha kuhiji ilihali mtu yuko na uwezo?

Jibu: Udhahiri ni kwamba ni dhambi kubwa. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ

”Kwa ajili ya Allaah ni wajibu kwa watu watekeleze hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo wa kuiendea. Na atakayekanusha, basi hakika Allaah ni mkwasi kwa walimwengu.”[1]

Bi maana kuipoteza hajj. Kwa msemo mwingine ameiacha hajj ilihali ni muweza. Ni jambo khatari na dhambi kubwa.

[1] 03:97

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23273/حكم-من-ترك-الحج-وهو-مستطيع
  • Imechapishwa: 16/12/2023