Swali: Mwanafunzi ameacha kujibu swali kwa ajili ya uchaji licha ya kwamba haitakiwi kuacha kujibu swali kama hilo.

Jibu: Haijuzu kufanya hivo isipokuwa ikiwa kama atamwelekeza muulizaji kwa mwengine. Ni sawa akimwelekeza muulizaji kwa mwingine kwa sababu ya uchaji au kwa sababu wengine wanajua zaidi kuliko yeye. Maswahabah walikuwa wakifanya hivo. Ama kuwaacha watu katika ujinga na kusema eti ni kwa ajili ya kumcha Allaah, huo sio uchaji. Ajitahidi ikiwa hakuna mwingine zaidi yake.

Ikiwa anayo shaka basi asijibu pasi na elimu. Ikiwa lengo lake ni uchaji na wapo wengine ambao ni wajuzi zaidi kuliko yeye, basi aelekeze kwao na awaambie wakamuulize mtu huyo.

Swali: Hadiyth ya Abu Hurayrah inayosema:

“Yule mwenye kuulizwa juu ya elimu akaificha, basi atapigwa hatamu ya Moto siku ya Qiyaamah.”[1]

Je, ni Swahiyh?

Jibu: Ndio.

Swali: Je, mtu ambaye anaulizwa juu ya kundi potofu akanyamaza anaguswa na Hadiyth hii?

Jibu: Ndio, anaingia ndani ya Hadiyth hii.

[1] Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (120).  

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22986/حكم-ترك-طالب-العلم-جواب-الساىل-تورعا
  • Imechapishwa: 03/10/2023