Swali: Mwenye kumsifu Allaah baada ya kufanya jambo la haramu kama vile kuvuta sigara, kunywa pombe au uzinzi kwa ajili kuichezea shere dini anakufuru?

Jibu: Ni jambo linatakiwa kuangaliwa vyema. Ikiwa malengo yake ni kuicheza shere dini na anamsifu Allaah wakati wa kufanya maasi na kuona kuwa hakuna tofauti ya kumshukuru Allaah wakati wa kufanya dhambi na kumshukuru wakati wa kupata neema ya kidini, ni kufuru kubwa. Kufanya maskhara na dini ni kufuru:

قُلْ أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ

“Sema:  Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayah Zake na Mtume Wake?”  Msitoe udhuru; mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.”[1]

Lakini ikiwa anamsifu Allaah kutokana na mtihani wake, kwamba yeye anatubu na kurejea kwa Allaah, anaona kuwa ni msiba, hivyo anamsifu Allaah wakati wa msiba kama anavomsifu wakati wa kupata neema, akamuomba Allaah msamaha na kumuomba amkubalie tawbah yake, huku sio kuichezea shere dini.

[1] 09:65-66

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22987/حكم-من-حمد-الله-عند-مواقعة-فعل-محرم
  • Imechapishwa: 03/10/2023