Kunuia I´tikaaf kila wakati mtu anapoenda kuswali msikitini

Swali: Baadhi ya watu wanapoingia Msikitini baada ya adhaana wananuia I´tikaaf baina ya adhaana na Iqaamah. Je, wanapata kufanya hivo?

Jibu: Hili ni jambo ambalo halikuthibiti kutokana na ninavyojua. Haikuthibiti ya kwamba mtu anapoenda kuswali ananuia kukaa I´tikaaf. Hata kama wanachuoni wa Fiqh wamesema kitu kama hichi, kama ilivyo katika Sharh Zaad na Sharh-ul-Muntahaa. Wanasema inatakikana akiingia Msikitini anuie I´tikaaf. Jambo hili hatujaona dalili yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (17) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-03-14.mp3
  • Imechapishwa: 14/11/2014