Ambayo Allaah anamneemesha kafiri hayatoki katika moja ya mambo mawili:
1 – Ima sababu yake ikawa ni utiifu ambao alifanya. Kafiri alimfanyia wema mtu mwengine. Allaah anamlipa duniani na anamuharakishia thawabu yake duniani. Kafiri anaweza kufanya baadhi ya wema na Allaah akamlipa duniani. Lakini Aakhirah hana fungu lolote.
Kuhusu muumini, huenda duniani asipate lolote kwa kuwa Allaah amemuwekea malipo yake Aakhirah. Anaweza pia kupata duniani na Aakhirah:
رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ
“Mola wetu Tupe katika dunia mema na katika Aakhirah [pia Tupe] mema na tukinge na adhabu ya Moto.” (02:201)
2 – Hilo linaweza kuwa pia ni kumvuta, si kutokana na wema wake, bali ni kutokana na kumvuta. Allaah (Ta´ala) anasema:
وَلَا يَحْسَبَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا أَنَّمَا نُمْلِي لَهُمْ خَيْرٌ لِّأَنفُسِهِمْ ۚ إِنَّمَا نُمْلِي لَهُمْ لِيَزْدَادُوا إِثْمًا ۚ وَلَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ
“Na wala wasidhanie kabisa wale ambao wamekufuru kwamba muhula Tunaowapa [wa kustarehe] ni kheri kwa nafsi zao. Hakika tunawapa muhula ili wazidi [kufanya] dhambi. Nao watapata adhabu ya kudhalilisha.” (03:178)
أَيَحْسَبُونَ أَنَّمَا نُمِدُّهُم بِهِ مِن مَّالٍ وَبَنِينَ نُسَارِعُ لَهُمْ فِي الْخَيْرَاتِ ۚ بَل لَّا يَشْعُرُونَ
“Je, wanadhani kwamba kwa vile Tunavyowakunjulia kwa mali na watoto. Tunawaharakishia katika ya kheri? Bali hawahisi.” (23:55-56)
وَلَا تَمُدَّنَّ عَيْنَيْكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعْنَا بِهِ أَزْوَاجًا مِّنْهُمْ زَهْرَةَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا لِنَفْتِنَهُمْ فِيهِ ۚ وَرِزْقُ رَبِّكَ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ
“Na wala usikodolee macho yako kwa yale Tuliyowastareheshea baadhi ya watu miongoni mwao, kwani hayo ni mapambo ya maisha ya dunia tu ili tuwafitinishe kwavyo. Na riziki ya Mola wako ni bora zaidi na ni yenye kubakia.” (20:131)
فَلَمَّا نَسُوا مَا ذُكِّرُوا بِهِ فَتَحْنَا عَلَيْهِمْ أَبْوَابَ كُلِّ شَيْءٍ حَتَّىٰ إِذَا فَرِحُوا بِمَا أُوتُوا أَخَذْنَاهُم بَغْتَةً فَإِذَا هُم مُّبْلِسُونَ
“Waliposahau yale waliyokumbushwa nayo, Tuliwafungulia milango ya kila kitu [walichotaka], mpaka walipofurahia kwa yale waliyopewa, tukawachukua ghafla [tukawaadhibu], basi mara wao wakawa wenye kukata tamaa.” (06:44)
Allaah anawavuta. Kama alivyosema Allaah (Ta´ala):
فَذَرْنِي وَمَن يُكَذِّبُ بِهَـٰذَا الْحَدِيثِ ۖ سَنَسْتَدْرِجُهُم مِّنْ حَيْثُ لَا يَعْلَمُونَ
“Basi Niache na anayekadhibisha hadithi hii [Qur-aan], Tutawavuta pole pole kwa namna wasiyoijua.” (68:44)
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Iqtidhwaa’-is-Swiraat al-Mustaqiym (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ektda–1429-12-8.mp3
- Imechapishwa: 05/05/2015

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Iqtidhwaa’-is-Swiraat al-Mustaqiym (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ektda–1429-12-8.mp3
Imechapishwa: 05/05/2015
https://firqatunnajia.com/kuneemeshwa-kwa-kafiri-duniani/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)