Suufiyyah wanaonelea kuwa makusudio ni Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Mtu akihakikisha Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah, bi maana mtu akishuhudia ya kwamba hakuna anayeendesha mambo, anayeumba na kuruzuku isipokuwa Allaah, basi huyu ndio Muislamu kwa mujibu wao hata kama hakumuabudu Allaah, hakuswali na kutoa zakaah. Haya ndio madhehebu yao batili na tunaomba kinga kwa Allaah. Wanaonelea vilevile kuwa hakuna neno akafanya machafu kwa kuhalalisha mambo ya haramu kwa kuwa wanaonelea kuwa anakubali Tawhiyd, nayo ni kuthibitisha kuwepo kwa Mola.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ektda–1430-4-22.mp3
  • Imechapishwa: 05/05/2015