Kunakhofiwa amesaidia kujiua nafsi yake

Swali: Je, anaingia [katika waliojiua nafsi zao] ambaye anakimbiza gari kwa kasi isiyokuwa ya kawaida kisha baadaye gari likampindukia?

Jibu: Kunakhofiwa juu yake kwamba amesaidia kuiua nafsi yake. Kunakhofiwa juu yake kupata dhambi. Hapana shaka kwamba ni mwenye kupata dhambi kwa kuvuka mipaka. Anakuwa ameshirika kuiua nafsi yake.

Swali: Aliyegongwa na gari anaingia katika waliokufa mashahidi?

Jibu: Ndio, Allaah akitaka. Aliyegongwa ni katika sampuli za watu waliyoporomokewa na jengo au ni mbaya zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22932/حكم-ما-يقع-للمسرع-بالسيارة-وحكم-المصدوم
  • Imechapishwa: 16/09/2023