Kuna wakati maalum unaotakiwa kuwekwa baina ya kukimu na kuswali?

Swali: Je, kuna kikomo kipambanuzi kati ya iqaamah na swalah?

Jibu: Hakuna kikomo maalum. Muhimu iwe kitu kisichowadhuru watu. Asiharakishe ili watu waweze kuwahi. Isipokuwa inapokuja katika Dhuhr wakati wa jua kali bora ni kuchelewesha. ´Ishaa pia kama hawajakusanyika bora ni kuchelewesha. Nyakati zilizosalia wazingatie wakati unaofaa kwa mfano robo saa, dakika ishirini, theluthi moja ya saa ili watu waweze kuwahi. Hakuna kikomo maalum. Awafanyie upole.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23712/ما-مدة-الفصل-بين-الاقامة-والصلاة
  • Imechapishwa: 08/04/2024