Kuihesabu Rak´ah ya Sunnah katika zile Rak´ah za faradhi alizoswali mtu

Swali: Ibn Hazm amesema:

“Ambaye yuko anaswali Sunnah kisha kukakimiwa swalah ya mkusanyiko basi ajiunge nao. Akiwa kwa mfano ameshaswali Rak´ah moja basi aketi mwishoni mwa swalah yake mpaka aikidhi ile Rak´ah ambayo amekwishaiswali.”?

Jibu: Hapana, hili halina msingi. Anachotakiwa ni ima kuikata swalah hiyo ya kujitolea au aikamilishe na kujiunga pamoja nao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23714/حكم-من-اقيمت-الصلاة-وهو-يصلى-نافلة
  • Imechapishwa: 08/04/2024