Kuna tofauti nyingi kati ya Shiy´ah na Ahl-us-Sunnah

Swali: Naomba uniwekee wazi tofauti kati ya Ahl-us-Sunnah na Shiy´ah na pote lililo karibu zaidi katika Sunnah?

Jibu: Tofauti zilizopo kati ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na Shiy´ah ni nyingi katika yanayohusiana na Tawhiyd, utume, uongozi na mengineyo.

Wanachuoni wengi wameandika kuhusu hilo. Baadhi yao ni Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah katika “Minhaaj-us-Sunnah”, “al-Milal wan-Nihal” cha ash-Shahrastaaniy, “al-Fiswal” cha Ibn Hazm, “al-Khutwut al-´Ariydhwah” na “al-Mukhtaswar at-Tuhfah al-Ithnaa ´Ashariyyah” vya Muhibb-ud-Diyn al-Khatwiyb. Juu ya hilo rejea vitabu vilivyotajwa.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/266-267)
  • Imechapishwa: 23/08/2020