Kuna dalili inayokataza mahari yasiwe makubwa?

Swali: Je, kuna dalili katika Sunnah inayokataza ukubwa wa mahari?

Jibu: Kakataza ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) mahari makubwa. Bora zaidi mahari yawe madogo kwa kufuata Sunnah. Hakika ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) anasema:

“Hakuzidisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika mahari ya mke wake wala mabanati zake zaidi ya dirhamu tano.” (Hadiyth hii imepokelewa na Muslim)

Uongofu bora ni uongofu wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Atakayezidisha na akawa anaweza hilo hakuna ubaya. Kama alivyosema Allaah:

“Mkitaka kubadilisha mke mahali pa mke, na hali mmoja wao mmempa chungu ya mali, basi msichukue katika hayo kitu chochote.” (04:20)

Nukta muhimu:

”Na hali mmoja wao mmempa chungu ya mali.” (04:20)

Ikiwa anaweza hakuna ubaya. Wala watu hawahukumiwi hukumu moja, fulani alitoa kiwango fulani nawe toa kiwango fulani. Fulani anaweza kuwa na uwezo, na huyu mwengine akawa hana uwezo.

Check Also

Kufanya sherehe inapoisha nifasi ya mwanamke siku arubaini

Swali: Ipi hukumu ya “al-Arba´iyniyyah” yaani mwanamke mwenye nifasi damu yake inapokatika na akatwahirika damu …