Kaoa mwanamke wa Ahl-ul-Kitaab ambaye hataki kuingia katika Uislamu

Swali: Nimeoa mwanamke wa Ahl-ul-Kitaab kabla ya kuwa na msimamo, na nimepewa fatwa na baadhi ya wanafunzi kuwa na subira nae mpaka hapo atapoingia katika Uislamu, na kumeshapita miaka mitatu na bado hajaingia katika Uislamu na sina nae watoto, na kwa sasa niko na matatizo nae, ipi nasaha zako?

Jibu: Bila wasiwasi wowote Shari´ah inajuzisha kuoa mwanamke wa Ahl-ul-Kitaab hata kama hatosilimu. Inajuzu kwake hilo. Kwa dalili ya Qur-aan. Ama kuhusiana na matatizo hilo ni jambo la kawaida hata baina ya mume na mke ambao ni Waislamu, na baina ya hawa Ahl-ul-Kitaab.

Ni juu yake kuangalia ambavyo anaweza kupatana nae ikiwa bado anataka kubakia nae, na ikiwa matatizo yao haikuwezekana, itakuwa ni kama Alivyosema Allaah atampa Allaah kila mmoja wasaa wake.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2280
  • Imechapishwa: 22/09/2020