Baba hataki kuwaozesha mabinti zake kwa kukhofia riziki zao

Swali: Ipi hukumu ya baba ambaye hataki kuwaozesha mabinti zake kwa ajili ya riziki zao?

Jibu: Huchukuliwa kuwa ni dhalimu. Allaah hawapendi madhalimu. Allaah amesema:

وَالظَّالِمِينَ أَعَدَّ لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا

”Wenye kudhulumu amewaandalia adhabu iliyo chungu.” (76:31)

Riziki yao iko kwa Allaah. Akimuozesha binti yake riziki yake iko kwa Allaah. Ajitahidi kumuozesha kwa mwanamume mwema ambaye atamsaidia katika dini na dunia yake. Haijuzu kwake kumkatalia kwa kitu alichomhalalishia Allaah.

Check Also

Mwanamke hana Adhaana wala Iqaamah

Swali: Ikiwa ataadhini mwanamke nyumbani kwake, au mwalimu mwanamke madrasani kwake… Jibu: Hakuna adhaana kwa mwanamke. …