Swali: Je, Iqaamah ni kama adhaana kwa maana ya kwamba mtu anatakiwa kusema kama anavosema muadhini?

Jibu: Iqaamah ni kama adhaana. Ni adhaana ya pili. Lakini wakati wa kukimu mwitikiaji aseme (قد قامت الصلاة) na wakati wa al-Haylah aseme ( لا حول ولا قوة إلا بالله). Sehemu hizi aseme kama anavosema mwenye kukimu. Bali anatakiwa kusema ( لا حول ولا قوة إلا بالله). Wakati wa kukimu aseme (قد قامت الصلاة). Imekuja katika baadhi ya Hadiyth kwamba mwitikiaji aseme:

أقامها وأدامها

“Ameisimamisha na kuitekeleza.”

Hata hivyo ni dhaifu. Maoni ya sawa ni kwamba mwitikiaji aseme (قد قامت الصلاة) kama anavosema muadhini.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22499/هل-يردد-في-الاقامة-مثل-ما-يردد-في-الاذان
  • Imechapishwa: 04/07/2023