Swali: Ni lazima kwangu kuomba haki yangu ikiwa nitaudhiwa wakati wa kuamrisha mema na kukataza maovu?

Jibu: Usiombe haki yako. Subiri. Ukiomba haki yako itakuwa unainusuru nafsi yako. Subiri juu ya hili. Isipokuwa yakikiukwa yale aliyokataza Allaah basi hapo ndipo utaomba aadhibiwe yule aliyekeuka mipaka ya Allaah. Kuhusu ambaye amekufanyia mabaya fanya subira kwake:

يَا بُنَيَّ أَقِمِ الصَّلَاةَ وَأْمُرْ بِالْمَعْرُوفِ وَانْهَ عَنِ الْمُنكَرِ وَاصْبِرْ عَلَى مَا أَصَابَكَ

“Ewe mwanangu! Simamisha swalah, na amrisha mema, na kataza maovu na subiri kwa yanayokupata.”[1]

[1] 31:17

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (01)
  • Imechapishwa: 11/02/2024