Swali: Vipi tutaoanisha kati ya maneno Yake Allaah (Ta´ala):

وَلَقَدْ آتَيْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ وَرَزَقْنَاهُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ وَفَضَّلْنَاهُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ َ

”Hakika Tuliwapa wana wa israaiyl Kitabu na Hekima na unabii na tukawaruzuku katika vizuri na tukawafadhilisha juu ya walimwengu.”[1]

na:

كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ

“Mmekuwa Ummah bora kabisa ulioteuliwa kwa watu – mnaamrisha mema na mnakataza maovu na mnamwamini Allaah.”[2]?

Jibu: Ndio, walifadhilishwa katika wakati wao. Ni kweli kwamba wao ndio bora wa watu wa wakati wao. Wana wa israaiyl ndio wabora wa watu wa zama zao. Kuhusu kusema kwamba wao ndio bora wa walimwengu mzima, hapana. Lakini  ni kweli kuwa wao ndio bora wa watu wa wakati wao. Wengi wao ni waumini. Msingi wao ni waumini. Wao sio kama waabudia mizimu.

[1] 45:16

[2] 03:110

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (02)
  • Imechapishwa: 11/02/2024