Swali: Du´aa ifuatayo:

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba kwa maeneo haya matukufu au kwa saa hii tukufu au kwa usiku huu mtukufu.”

Ni du´aa inayoruhusiwa?

Jibu: Ikiwa maeneo hayo ni matukufu kweli kwa mfano wa msikiti Mtakatifu, msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), msikiti wa al-Aqswa, ´Arafah, Minaa na Muzdalifah ni sawa. Unamuomba Allaah mahala hapa ya kwamba Allaah akukubalie na akusamehe. Na ni sawa kuomba kwa saa hii yenye kuitikiwa kama mfano mwishoni mwa usiku na wewe huku umesujudu mbele ya Allaah. Haya ni matendo ambayo unatawassul kwayo kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (23) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2135
  • Imechapishwa: 11/07/2020