Swali: Mwenye kusema “Ee Allaah! Hakika mimi ninatawassul Kwako kutokana na ninavyokufanyia mapungufu” ni sahihi?

Jibu: Tawassul kwa Allaah kwa udhaifu na haja yako. Usisemi kwa upungufu. Upungufu sio utiifu. Upungufu sio utiifu ambao mtu anatawassul nao kwa Allaah. Badala yake watakiwa kusema “Ee Allaah! Mimi nina mapungufu na makosa.” Usitawassul kwa Allaah kwa mapungufu yako. Unachotakiwa ni kutawassul kwa Allaah kutokana na udhaifu na kule kumuhitajia Kwake (Subhaanah) pamoja vilevile na kukubali ya kwamba wewe ni mfanya mapungufu. Ukubali ya kuwa wewe ni mfanya mapungufu. Kukiri kwako ya kwamba wewe ni mfanya mapungufu ni ´ibaadah na matendo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (23) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2135
  • Imechapishwa: 11/07/2020