Kumuokota mnyama aliyepotea na kumtangaza mwaka mmoja

Swali: Je, wanyamahoa waliopotea wanapaswa kutangazwa?

Jibu: Ndiyo, kwa mwaka mmoja. Yeyote anayeokota mnyama aliyepotea, yeye mwenyewe ni mpotevu asipomtangaza. Hili linahusu wanyamahoa tu. Ama ngamia, anapaswa kumwacha, pamoja na ng’ombe, farasi na punda.

Swali: Nini maana ya maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Huyo ni wako, mwenye nao au wa mbwa mwitu.”?

Jibu: Inamaanisha kwamba anapaswa kumtangaza. Usimwache aliwe na mbwa mwitu. Mchukue na mtangaze.

Swali: Je, mtu anapata dhambi ikiwa hakumchukua mnyamahoa kwa sababu ya kuchelea majukumu?

Jibu: Hapana, hapati dhambi. Mnyamahoa huyo ni halali kwake:

”Ni wako, wa ndugu yako au wa mbwa mwitu.”

Lakini kwa sharti la kumtangaza.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25420/حكم-اخذ-ضالة-الغنم-ومدة-تعريفها
  • Imechapishwa: 24/03/2025