Kuokota pesa na kuzikabidhi shirika la misaada kwa nia ya mmiliki wake

Swali: Vipi ikiwa mtu ameokota pesa barabarani na akaikabidhi kwa shirika la misaada kwa nia ya kuitolea swadaqah kwa niaba ya mmiliki wake?

Jibu: Hapana, haifai. Ni lazima aitangaze au aikabidhi kwa mamlaka inayohusika na mali iliyopotea. Ikiwa kuna mamlaka inayoshughulikia vitu vilivyopotea, basi aiwasilishe huko. Vinginevyo ni lazima atangaze mali hiyo.

Swali: Je, kutoa ushahidi ni wajibu?

Jibu: Kwa mujibu wa Hadiyth linaonekana kuwa ni wajibu, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“… basi na ashuhudishe.”

Msingi wa amri katika Shari´ah inapelekea katika ulazima. Hata hivyo kuna maoni kuwa huenda ikawa ni jambo linalopendekezwa tu, kwa kuwa katika Hadiyth ya Zayd bin Khaalid iliyopokewa na al-Bukhaariy na Muslim na Hadiyth nyingine nyingi hakuna amri ya lazima ya kushuhudisha. Kwa hiyo inaweza kusemwa kwamba hilo makusudio ya kushuhudisha ni kwa njia ya mapendezo na ubora.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25422/حكم-من-وجد-مالا-وسلمه-لجهة-خيرية-بنية-الصدقة
  • Imechapishwa: 24/03/2025